User:Haji

From WikiEducator
Jump to: navigation, search

Self introduction

Jina langu ni Haji Khamis Fundi, nimezaliwa kijiji cha Kitogani, Wilaya ya Kusini katika kisiwa cha Unguja katika mwaka 1954. Mimi ni mtoto wa kwanza katika familia ya watu wanne.

Nilianza masomo ya Msingi katika Skuli ya Kitogani na kumalizia Sekondari ya Lumumba, Zanzibar katika mwaka 1975. Kwa bahati nilipata nafasi ya kwenda mafunzo ya Kilimo na Udaktari wa Mifugo katika chuo cha Kilimo cha Ukirighetiuru, Mwanza Tanzania mnamo mwaka 1978 ambako nili pata cheti cha Kilimo. Katika mwaka 1980 nilipata Diploma ya Maendeleo Vijijini huko nchini Cameroon; na baadae nilipata Shahada ya Uzamili ya Kilimo nchini Bulgaria katika mwaka 1988.

Hivi sasa mimi ni mfanyakazi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo, Zanzibar. Leo niko katika mafunzo ya Web 2.0 ambayo yatamalizika siku ya Ijumaa na ninategemea kupata cheti cha mahudhurio.

Ahsante